QUALITY ANIMAL FEEDS
Chakula cha kuku na ng’ombe
cha KIBOKO ni chakula chenye Ubora wa hali ya juu na kinatengenezwa kwa
kuzingatia maadili yote ya Uzalishaji yanavyopaswa kutekelezwa.
Aina
ya vyakula:
1. Kuku wa nyama (Broilers):
BROILER STARTER
BROILER FINISHER
2. Kuku wa mayai (Layers):
CHICK MASH
GROWERS MASH
LAYERS MASH
3. Dairy Meal (Ng’ombe wa Maziwa):
Matumizi:
1.
Kuku wa nyama (Broilers):
Broilers- watachukuwa muda wa takriban wiki NNE pekee wakilishwa chakula cha
KIBOKO ANIMAL FEEDS.
Chakula- wiki 1-2.5 wape Broiler Starter bila kuwapimia na maji safi ya
kunywa ya kutosha.
- wiki 2.5-4 wape Broiler
Finisher mpaka washibe na pia maji safi wakati wote.
ZINGATIA CHANJO
NA USAFI WA BANDA NA MAZINGIRA IPASAVYO KWA MATOKEAO BORA NA FAIDA.
2.
Kuku wa mayai (Layers):
Layers – watachukua muda wa kati ya wiki 16 hadi 20 kuanza kutaga.
Chakula- wiki 1 – 6 wape Chick Mash ya kutosha na maji safi.
-Wiki 6 – 16 wape
Growers Mash ya kutosha na maji safi ya kunywa kila wakati.
- Wiki 16 na kuendelea wape Layers Mash kwa ajili ya kuanza kutaga na
kuendelea
pamoja na maji safi ya kunywa kila wakati.
CHANJO NA USAFI
NI MUHIMU SANA KWA MATOKEO BORA KWA UFUGAJI WA FAIDA.
MAMBO
MUHIMU:
ü Zui watu wasiohusika, kuku na ndege kuingia au kukaribia mabanda
yako.
ü Hakikisha banda lipo katika mazingira safi yasiyofurika au kutuama
maji.
ü Ondoa mbolea mara kwa mara ikiwa ndani ya mifuko na tupa mbali na
eneo la mabanda.
ü Wafanyakazi wote wabadilishe nguo na wawe safi. Wasafishe mikono na
miguu yao kila wakati waingiapo mabandani kwa kutumia dawa.
ü Dawa ikwekwe kwenye maji ya mlangoni ili kutumbukiza miguu kabla ya kuingia bandani na
kubadilishwa kila wiki.
ü Mabanda yapumzishwe wiki mbili kabla ya kuwekwa kuku wapya.
ü Kabla ya kuweka kuku wapya, safisha mabanda kwa kutumia dawa na
ufunge banda kwa muda wa siku saba.
JINSI YA KUSAFISHA NA KUPIGA DAWA MABANDA KABLA YA KUINGIZA KUKU
(FUMIGATION)
Ondoa mbolea na vitu vyote vilivyotumika
(mifuko ya chukula, makopo, n.k) na kuitupa mbali kabisa na mabanda yako.
ü Anza kusafisha dari, halafu kuta na kumalizia na sakafu.
ü Loweka vyombo vya kunywea maji
na kulishia chakula na vifaa vyote vinavyotumika ndani ya mabanda kwenye dawa kwa muda wa nusu saa
halafu suuza na maji ya kawaida.
ü Piga dawa ya wadudu warukao na watambaao ndani na nje ya banda.
ü Weka dawa kwa FOOTBATH… mlangoni kabla ya kuleta vifaranga.
KUDHIBITI KUSAMBAA MAGONJWA NDANI YA MABANDA.
ü Osha vyombo vya kunywea maji kila unapoweka maji mpya.
ü Loweka vyombo kwenye dawa kwa muda wa nusu saa angalau mara moja kwa
wiki.
ü Badili maji yenye dawa mlangoni
mara moja kwa wiki.
ü Kama unatumia maji yasiyo salama, weka dawa ya kuua vimelea vya
magonjwa. Kumbuka maji salama kwa kuku ni yale ambayo hata wewe mfugaji unaweza
kuyanywa.
ü Jiepushe na vyakula vyenye mahindi na dagaa walihoribika kwa sababu
ni chanzo cha sumu ya mycotoxins ni hatari kwa kuku.
MAGONJWA
YA KUKU WA MAYAI.
NA.
|
MAGONJWA
|
DALILI
|
CHANJO/TIBA
|
1.
|
New Castle Disease (Mdondo).
|
-
Vifo vingi vya ghafla.
-
Kuharisha.
-
Hutokea wakati wowote baada
ya wiki mbili.
|
Chanjo siku ya 7, rudia siku ya 21
kila baada ya wiki 12.
|
2.
|
Gumboro.
|
-
Vifo vya ghafla
-
Kukunja mabawa chini.
-
Kujikusanya pamoja.
-
Kuharisha kinyesu cheupe.
-
Ugonjwa hutokea kuanzia wiki
ya 2 hadi 18.
|
Chanjo siku ya 10 – 14, rudia siku ya
28 na 42 kwa kuku wa mayai.
|
3.
|
Avian Leukosis Complex.
|
-
Mavecks – humpata kuku
kuanzia umri wa wiki tatu, lakini mara nyingi ni wiki ya 12 – 24.
-
Dalili ni kupooza mabawa,
kuvimba na kufa.
-
Kuvimba miguu, maini, wengu
na figo.
|
Tibu.
|
4.
|
Fowl Typhoid (kideli).
|
-
Vifo vya kuku mmoja mmoja.
|
Tibu.
|
5.
|
Pollorum.
|
-
Huuwa zaidi vifaranga wadogo
kuanzia siku ya kwanza hadi wiki tatu.
-
Vifaranga hujikusanya karibu
na chanzo cha joto na kusinzia na kutoka na uharo mweupe.
|
Zingatia usafi wa mabanda na tiba.
|
6.
|
Paratyphoid.
|
-
Dalili hazionekani, vifo
hutokea wiki ya kwanza vifaranga hudumaa, wachovu na wanaweza kuharisha.
|
Tibu.
|
7.
|
Colibacilosis.
|
-
Vifo wiki ya kwanza vitovu
havikauki.
-
Hushindwa kupumua.
-
Macho na kichwa kuvimba.
-
Tumbo hujaa maji (Ascitis).
|
Tibu.
|
8.
|
Colyza (majua)
|
-
Kupiga chafya.
-
Kutoa makamasi.
-
Kuvimba uso mara chache na
kupata pneumonia.
|
Tibu.
|
9.
|
Coccidiosis (kuharihsa damu)
|
-
Dalili zipo nyingi.
-
Kinyesi kuwa na rangi ya
ugoro au damu tupu.
-
Vifaranga kudumaa.
|
Tibu.
|
10.
|
Foul Pox (Ndui).
|
-
Kwa kuku wa mayai.
|
Kila kuku atachinjwa sahemu katika
mbawa. Endelea kuwapa maji ya vitamin.
|
MAGONJWA YA KUKU WA NYAMA:
NO.
|
MAGONJWA
|
DALILI
|
CHANJO/TIBA.
|
1.
|
New Castle (Mdondo).
|
-
Vifo vingi vya ghafla.
-
Kuharisha
-
Hutokea wakati wowote baada
ya wiki mbili.
|
Chanjo kwa masaa wawili tu endelea na
maji ya vitamin wiki ya kwanza.
|
2.
|
Gumboro.
|
- Vifo vya ghafla.
- Kukunja mabawa chini.
- Kujikusanya pamoja.
- Kuharisha kinyesi cheupe.
- Ugonjwa hutokea kuanzia wiki ya pili.
|
Chanjo kwa masaa mawili tu na endelea
na maji ya vitamin.
|
MAGONJWA YA MLIPUKO:
·
New Castle (Mdondo).
·
Gumboro.
3.
KIBOKO Diary Meal:
Chakula bora cha ng’ombe wa maziwa. Kilo
sita (6) tu kila siku zinatosha kumfanya ng’ombe wako atoe maziwa mengi na ya
kutosha.
·
Mpe kilo tatu (3) asubuhi na
tatu (3) jioni wakati wa kukamua.
·
Ng’ombe ale majani ya kutosha
na apewe maji safi na salama ya kunywa.
·
Ng’ombe apate chanjo kwa ajili
ya magonjwa ya mlipuko.
·
Mwogeshe ng’ombe wako mara kwa
mara kwa kutumia dawa.
·
Ng’ombe alale mahali pazuri na
pakavu.
ANGALIZO:
I.
Ng’ombe apate tiba kwa wakati.
II.
Ng’ombe apate dawa ya minyoo
kwa wakati.
KWA MAELEZO
ZAIDI WASILIANA NASI:
Ø Sai Energy and Logistic Services,
P.O.Box 333,
Iringa, Tanzania.
Ø Tel:-
: (026) 2725039, (026) 2725053
Ø Mobile
: 0712604888,
0763299664, 0786870697.
Ø Fax
: (0260 2725004.
No comments:
Post a Comment