Wednesday, April 1, 2015


UFUGAJI WA SAMAKI
Na Augustino Chengula
UTANGULIZI
Ufugaji wa samaki unahusisha kuwafuga samaki katika mazingira tengefu (yasiyo ya
asili kwenye mabwawa au matangi) na kuwavuna
kwa aajili
ya kula katika familia au
kuwauza sokoni.
Histor
ia ya ufugaji wa
viumbe
-
maji inaonekana kuwepo tangu enzi za zamani sana.
Kaitka maandishi ya mkono yaliyoandikwa na Wachina wa kale karne ya 5 kabla ya
Kristo yanaonyesha kuwa Wachina walikuwa wanafuga samaki. Historia pia
inaonyesha kuwa ufugaji mkubwa ulijaribiwa na Wa
misri wakati wa Ufalme wa kati
(2052
-
1786 kabla ya Kristo)
japo hauonyeshi kama walifanikiwa na ufugaji huo.
Ufugaji aina ya Kombe ulifuatiwa na Warumi ambao kumbukumbu zake ziliwekwa
vizuri na umeendelezwa katika njia tofauti hata katika nyakati za sasa.N
jia nyingi za
ufugaji wa samaki za zamani inatofautiana sana na njia tunazoziona leo hii na tofauti
kubwa ni kwamba zamani waliwavua samaki wadogo toka mazingira asili na
kuwahamishia katika mazingira yaliyotengenezwa kwa kufugia.
Ufugaji wa huu wa kisasa
ulianza kutumiwa mnamo mwaka 1733 pale ambapo
mkulima wa Kijermani alipofanikiwa kukusanya m
ayai ya samaki, akayarutubisha na
kuyaangua kisha samaki hawa watoto wakapelekwa kwenye matangi au
mabwawa
ya kufugia samaki.
Mwanzoni ufugaji huu ulifanyika kwenye maji baridi na samaki wa
maji baridi na baadaye karne ya 20 hivi ufugaji wa maji
-
chumvi kwa kutumia samaki
wa maji
-
chumvi ulianza kwa vile ujuzi mpya ulikuwa umegunduliwa.
Historia ya ufugaji wa samaki Tanzania hauj
awekwa vizuri kwenye maandishi, lakini
kulingana na
Balarin (1985) anasema majaribio yalianza mnamo mwaka 1949 katika
mikoa ya Tanga (Korogwe) na Mwanza (Maly) ikionyesha kujengwa pia kwa
mabwawa mengi ya samaki. Lakini mabwawa haya yaliishia kutofanya kaz
i
kwasababu ya kukosa usimamiaji mzuri, matumizi ya technolojia isiyosahihi pamoja
na matatizo mengine kama ya ukame na miundo mbinu mibovu. Kulingana
na ripoti
iliyotolewa na FAO mwaka 1968 ilionyesha kuwa Tanzania ilikuwa na mabwawa 8
000 ya kufugia sama
ki japo mengine yalikuwa madogo yenye uzalishaji kidogo
kulingana pengine na usimamizi mbovu.
Mwaka 1967 serikali ya Tanzania ilianzisha kampeni ya kuhamasisha ufugaji wa
samaki, lakini ilishindikana kwasababu ya mipango mibovu na usimamizi mbovu.
Mwaka 19
72 kwa mara ya kwanza ufugaji wa samaki ulipewa umuhimu
kisera japo
sharia ilitungwa mwaka 1970. Mwaka 1997 sera ya ufugaji wa samaki ilipitishwa
iliyoipa kipaombele ufugaji wa samaki.
Ufugaji wa samaki Tanzania kwa sehemu kubwa unafanywa kama kazi ya zia
da na
wafugaji 17 100 wanafanya ufugaji wa maji baridi na 3 000 wa maji chumvi.
Kuna
takribani
mabwawa 14 100 yaliyo maeneo mbalimbali ya nchi yetu na wafugaji wengi
wa wale wafugaji wadogo wenye mabwawa yenye ukubwa wa mita za mraba 150.
Mgawanyo wa mabwa
wa katika nchi yetu unategemea sana vitu vifuatavyo;
upatikanaji wa maji, ardhi inayofaa kwa ufugaji wa samaki, uelewa na uhamasikaji
wa jamii ukitegemeana na umuhimu kiuchumi wa ufugaji wa samaki.
Kuna maeneo
manne Tanzania ambako ufugaji
wa samaki
umesha
miri
kwa kiasi fulani
(
una
mabwawa yanayozidi 1000
),
nayo
ni Ruvuma (4 942), Iringa (3 137), Mbeya (1 176)
na Kilimanjaro (1 660).
Mbali na kwamba kuna aina nyingi sana za samaki
wanaofugwa duniani, lakini katika nchi yetu ya Tanzania ni aina kuu mbili
zin
azofugwa ambazo ni pelage au tilapia na kambale. Chaguo hili la wafugaji wengi
wa aina hizi limetokana na urahisi wa kuwafuga hawa samaki kwa vile mahitaji yao
si makubwa sana.
Kwa nini
Mtanzania
ufuge samaki?
Kuna upungufu mkubwa sana
wa protini duniania na hasa katika nchi zinazoendelea
ikiwemo Tanzania inayotokana kwa asilimia kubwa na vyakula vya aina ya nyama.
Upungufu huu wa protini ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kiafya ya binadamu
hasa watoto wado
go na vijana wa umri chini ya
miaka 25 ambao wanahitaji kukuwa
kwa haraka. Ugonjwa wa Kwashako
kwa watoto ndiyo matokeo ya upungufu wa
protini mwilini.
Pia matumizi ya samaki na hasa mafuta ya samaki ambayo ndo yanatumika sana
kuwanywesha watoto wadogo yamethibitika kisayansi kuwa yana
saidia sana ukuaji
wa ubongo wa mwanadamu. Lakini pia uwepo wa kiwango kidogo sana cha
kolestero ambayo imeripotiwa kusababisha ugonjwa wa moyo kimepelekea
ongezeko la watu wanakula samaki.
Sababu zifuatazo hapa chini zinatoa jibu la kwa nini Mtanzania ufu
ge samaki;
-
Ongezeko kubwa la uhitaji wa samaki ndani na nje ya nchi yetu kunakofanya
samaki waliopa sasa kutotosheleza mahitaji.
-
Kupungua kwa samaki asili kwenye mito, maziwa na bahari kunakotokana na uvuvi
wa kupindukia na haramu.

No comments:

Post a Comment