Wednesday, April 1, 2015



SOMO 1 UTANGULIZI
FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU
a)    Chakula – nyama ya kuku na mayai hutumika kama Chakula minimum cha wanadamu
b)   Chanzo cha kipato – Mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai
c)    Chanzo cha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii
d)   Mbolea – kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao
e)    Shughuli za utafiti – kuku wanatumika katika tafiti nyingi za Baiologia kama kutambua mambo ya lishe.
f)     Shughuli za viwandani:
·         Mayai yenye mbegu ya jogoo hutumika katika kutengeneza dawa za chanjo
·         Magamba ya mayai yanaweza kutumika katika utengenezaji wa vyakula vya wanyama
·         Kiini cha njano cha mayai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya kuoshea nywele (shampoo0
g)   Kutunza kuku kwaajili ya kizazi kijacho ili kizazi kijacho kiweze kuona kuku ni lazima hivi sasa waendelee kufugwa.

VIKWAZO KATIKA UFUGAJI KUKU
a)    Chakula mara nyingi vyakula vya kuku vinakuwa vyenye ubora hafifu na hata upatikanaji wake huwa si mzuri
b)   Magonjwa – magonjwa kama mdonde au ndui huathiri ufugaji wa kuku. Ni vema magongwa kama hayo yakingwe au kuzuiwa ili kuendeleza ufugaji
c)    Mtaji – mara nyingine mtaji huwa kikwazo lakini endapo mikopo midogo midogo itatolewa kwa vikundi vitakavyo kuwa tayari na ufugaji utaendelezwa
d)   Madawa ya kuku – gharama za madawa ya kuku ziwe chini ili kuendeleza ufugaji.
e)    Tabia na miiko ya Jamii – baadhi ya jamii za makabila hapa chini, ufugaji wa kuku huona kama ni kitu duni hivyo basi jamii hizo zishawishiwe ili ziweze kuweka mkazo katika ufugaji wa kuku kwa nia ya kujiongezea kipato na kupata lishe bora pamoja na ajira.




SOMO LA 2  SIFA ZA KUKU WA KIENYEJI
SIFA
    1.        Wana uwezo wa kuatamia mayai yao na kuangua vifaranga
    2.        Wana uwezo wa kujitafutia Chakula ardhini lakini ili kuwaendeleza ni minimum wakaandaliwa Chakula bora na cha kutosha.
    3.        Wana uwezo wa kujilinda na maadui zao kama mwewe
    4.        Wavumilivu wa magonjwa mengo ya kuku lakini ni minimum wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku kama mdonde, ndui ya kuku

Ili kuweza kuwaendeleza:
Ni minimum kuku wao wakapewa mafunzo mazuri. Wawekwe kwenye mabanda mazuri wapewe maji na Chakula cha kutosha.

SOMO LA 3 MFUMO YA KUZALISHA KUKU
A:  Mfumo wa ufugaji huria
Huu ni mfumo rahisi lakini si mzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi. Katika kutumia mfumo huu kuku hufugwa ndani wakati wa usiku na kuachiwa huru wakati wa mchana ili kujitafutia Chakula.



Faida zake:
    1.        Gharama ndogo za ujenzi wa nyumba.
    2.        Gharama za Chakula hupungua kwani kuku huokota wadudu na kula baadhi ya majani
    3.        Gharama za kujenga uzio hazihitajiki
    4.        Kuku wa aina au umri wowote wanaweza kufugwa kwa mfumo huu.

Hasara za mfumo huu:
    1.        Uwezekakano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche au kuibiwa mitaani na kukanyagwa na magari
    2.        Kuku hutaga popote na upotevu wa mayai ni mkubwa
    3.        Kuna usimamizi hafifu wa kundi la kuku
    4.        Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa ya kuku
    5.        Utagaji unakuwa si mzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa
    6.        Uwekaji wa kumbukumbu si mzuri na mara nyingi kumbukumbu si sahihi.

Utumiaji mzuri wa mfumo huu:
    1.        Wajengee banda kuku kwa ajili ya nyakati za usiku na endapo hali ya hewa inakuwa si nzuri
    2.        Kuku wapatiwe Chakula na maji
    3.        Kuku wapatiwe viota vya kutagia
    4.        Kuku 100 watumie eneo la ardhi la ½ ha.



MFUMO WA NUSU NDANI NA NUSU NJE
Katika kutumia mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda yenye hewa ya kutosha na kuwe na uzio wenye majani. Uzio unaweza kujengwa kwa kutumia nyaya zenye matundu au miti.

FAIDA ZA MFUMO HUU:
1.    Tabia mbaya za kuku kama vile kudonoana si nyingi
2.    Mfumo huu hutumika kwa kuku wenye umri wowote
3.    Utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na ule wa huria

Hasara za mfumo huu:
1.    Unahitaji gharama za uzio
2.    Si nzuri kwa kuku wa nyama
3.    Matumizi ya muda mrefu ya eneo husika laweza kuwa na minyoo au vemelea vingine vyovyote vya magonjwa
Utumiaji mzuri wa mfumo huu
1.    Fanya usafi wa eneo husika na banda kila siku
2.    Ikiwezekana kuwe na mzunguko wa kutumia eneo hilo

c. MFUMO WA KUTUMIA MABANDA YENYE MATANDIKO:
Katika kutumia mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo yana sakafu au la, eneo la ndani hufunikwa na matandiko ya makapi ya mpunga, au takataka za mbao au maganda ya karanga.

FAIDA ZA MFUMO HUU
1.    Ni mzuri kwenye maeneo yenye ardhi haba
2.    Uangalizi wa kuku ni mzuri na ni rahisi
3.    Mchanganyiko wa vitamin B hutengenezwa katika matandiko hayo
4.    Hakuna haja ya kufagia vinyesi vya kuku kila siku
5.    Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuuwa vimelea vya maradhi
6.    Kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine
7.    Ni rahisi kukinga maradhi ya kuku
8.    Uwekaji wa kumbukumbu ni rahisi

HASARA ZA MFUMO HUU
1.    Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubwa
2.    Gharama za ujenzi wa mabanda zinahitajika

UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU:
1.    Matandiko yageuzwe kila siku
2.    Sehemu ya matandiko iliyomwagikiwa na maji izolewe
3.    Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha ambayo itatoa unyevu nyevu, hewa chafu pamoja na ammonia
4.    Mita mraba moja hutosha kwa kuku 5-8


Dhumuni kuu ni kupata kundi la kuku litakalofaa kwa sifa zote katika uzalishaji
Vipengele vya kuzingatia katika kuchagua kuku:
·         Utoaji wa mayai kwa mwaka uwe mzuri
·         Umbile la mwili na jinsi aonekanavyo
·         Uvumilivu wa maradhi, hii ni sawa na kuwa na vifo vichache
·         Uwezo wa kuotesha manyoya haraka
·         Uwezo mkubwa mwilini wa kutengeneza Chakula kuwa mayai au nyama
·         Ulaji wa Chakula uwe mdogo ukilinganisha na uzalishaji wake
·         Utagaji uwe wa muda mrefu kabla ya kupumzika
·         Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea

Njia zitumikazo katika kuchagua
·         Kwa kuangalia kuku wenyewe kulingana na sifa zilizotajwa hapojuu
·         Kwa kufuatilia kumbukumbu za wazazi wa kuku unaotaka kuwachagua
·         Kwa kuangalia kumbukumbu za familia (kaka na dada)
KUCHAGUA KUKU WASIOFAA KWENYE KUNDI
·         Inasaidia kuongeza uzalishaji wa mayai
·         Inapunguza kulisha kuku ambao uzalishaji wake ni hafifu
·         Inapunguza uenezaji wa magonjwa ya kuku
·         Huongeza nafasi zaidi kwa kuku wazuri kwenye banda
·         Uwezekano wa kuuza kuku kama hao ni mkubwa kabla hawajafa.
LINI KUCHAGUA?
·         Mara tu wakitotolewa
·         Wakati wa ukuwaji
·         Shughuli ya kila siku
·         Kuku waanzapo kutaga
·         Uzalishaji ukishuka chini ya asilimia 50
·         Wakati kuku wakiangusha manyoya

UPANDISHAJI WA KUKU
·         Kuku wenye uzito mdogo temba 15 hadi 20 kwa jogoo mmoja
·         Kuku wenye uzito wa juu temba 10 hadi 15 kwa jogoo mmoja

MIFUMO YA UPANDISHAJI
·         Upandishaji wa kuku wa koo moja au walio karibiana kiuzawa
·         Upandishaji wa kuku wa koo au jamii tofauti
·         Uboreshaji wa kuku wa kienyeji kwa kutumia majogoo ya kisasa. Lengo ni kuhamisha sifa nzuri za jogoo kwa vizazi vifuatavyo.

Huu ni uanguaji unaofanywa na kuku kwa kuatamia mayai. Kwa kawaida kuku mmoja anaweza kuatamia mayai 12 hadi 15 kwa mara moja. Kuku awekewe mayai ya kuanguliwa wakati wa kuatamia ukifika.

FAIDA ZA UANGUAJI WA ASILI WA VIFARANGA
      (i)      Mashine za kuangulia hazihitajiki hivyo gharama yake huwa ni kidogo
     (ii)     Mfugaji hahitaji ujuzi maalumu katika kufanya shughuli hii.
    (iii)    Huhitaji kuchunguza sehemju za ndani za mayai kwa kutumia mwanga kama inavyofanyika katika uanguaji kwa kutumia mashine.
    (iv)    Huhitajiki kurekebisha joto, unyevunyevu. Hali ya hewa na hata kugeuza mayai kama inavyofanyika kwenye mashine
     (v)     Huhitaji kuajiri mtu wakati unatumia uanguaji wa asili wa vifaranga.

KUCHAGUA MAYAI KWA AJILI YA UANGUAJI WA ASILI WA VIFARANGA
Uanguaji huboreshwa zaidi kwa kuzingatia uchaguzi wa mayai yanayofaa kwa kutotolewa, epuka mayai yafuatayo:
    1.        Mayai madogo sana
    2.        Mayai yasiyo na umbile la kawaida
    3.        Mayai yenye mafuta matuta
    4.        Mayai yenye viini viwili vya njano
    5.        Mayai yenye matundu matundu mengi
    6.        Mayai ambayo hayana mbegu ya jogoo
    7.        Mayai yaliyotoka kwenye kundi la kuku waliozeeka mno
    8.        Mayai kutoka kwenye kuku wagonjwa
    9.        Mayai yaliyohifadhiwa visivyo
 10.        Mayai kutoka kwenye mitetea yenye majogoo machache kuliko inavyoshauriwa.

Matayarisho yakiota
Kiota kitayarishwe kabla ya kuku hajaanza kutaga. Ndani yak iota weka matandiko kiota kiwe safi na kinyunyuziwe dawa ya unga (sevin) ya kuua wadudu. Kila baada ya kuangua kiota kisafishwe kabla ya kutumika kwa kuku wengine.

Kumtayarisha kuku wa kuatamia
Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini siku mbili kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa. Utitiri au viroboto. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na wasitulie kwenye viota vyao hali hii husababisha kuanguliwa kwa vifaranga wachache. Ikiwa kuku wana wadudu hao wanyunyize dawa. Kuku kwa ajili ya kuatamia awe na tabia na uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga vingi.

Uwezo kutumia boksi au kikapu kutengeneza kiota cha kutamishia


Faida
·         Vifaranga vingi huweza kutotolewa kwa wakati mmoja
·         Joto, unyevu pamoja na hewa hudhibitiwa
·         Hali ya usafi ni nzuri
·         Mayai yasiyofaa yanaweza kutolewa wakati wowote kabla ya siku ya kutolewa vifaranga.
·         Vifaranga hupatikana kwa mpangilio



Hasara
·         Gharama za kuanzia na kuendeshea ni ghali
·         Ujuzi maalumu unahitajika
·         Uwezekano wa milipuko ya magonjwa upo endapo mayai yatatoka kwenye vyanzo vingi
·         Uzalishaji unaweza kusimama endapo mashine itaharibika
·         Kutakuwa na gharama za ujenzi wa nyumba kwa ajili ya kuwekea mashine

Mahitaji minimum katika kutotoa mayai kwa kutumia mashine
1.   HALI YA JOTO
Joto linalohitajika kwenye mashine ni kati ya nyuzi 370c had 39Oc

2.   UNYEVUNYEVU
Yai linaweza kupoteza unyevunyevu kati ya asilimia 11 hadi 13 wakati liko kwenye mashine. Hivyo basi ili kuzuia maji mengi yasipotee kwenye yai ni lazima kwenye mashine kuwe na kifaa cha kuwekea maji. Unyevunyevu unaohitajika kwenye mashine ni asilimia 70 – 75 hadi siku ya ishirini na kupunguzwa hadi asilimia 50 baada ya vifaranga kuanguliwa ili vipate kukauka.
3.   HEWA SAFI
Kunatakiwa kuwe na chanzo cha hewa safi kwa ajili ya mayai yaliyomo kwenye mashine. Panga boi au matundu hutumika kwa shughuli hii

4.   Kugeuza mayai
Mayai hugeuzwa kwa siku 18 za kwanza. Lakini yasigeuzwe kwa kipindi cha masaa 24 ya kwanza. Mashine ambazo zina kifaaa cha kugeuza mayai pekee hugeuza mayai kila baada ya saa moja lakini ugeuzaji wa mayai kwa mikono hufanyika mara tatu au tano kwa siku.

Kuchagua vifaranga
Baada ya vifaranga kutotolewa inabidi kuchagua vifaranga ambavyo havina dosari. Vifaranga vyenye dosari vitolewe navyo ni vile ambavyo ni vidogo sana vilema na vile vyenye vitovu vibichi

Kufusha mashine za kutotolea
Ili kuua vimelea vya maradhi mashine za kutotolea hufushwa baada ya kusafishwa na wakati wa kuweka mayai mapya. Lakini usifushe mashine mnamo saa 96 (ambavyo ni sawa na siku nne) baada ya kuweka mayai kwenye mashine, kwani huu ni wakati ambao moyo wa kifaranga unaanza kufanya kazi. Tumia gram 114 za formalin kwa gram 85 za potassium permanganate katika kila ujazo wa mita 3 (3m2) za mashine.

Maandalizi minimum kabla ya kutunza au kupokea vifaranga;
-      Maandalizi muhimu kabla ya utunzaji au upokeaji wa vifaranga yafanyike wiki mbili kabla ya mapokesi ili kuepuka maandalizi ya haraka haraka
-      Endapo chumba au banda lilikuwa ikitumika kutunzia kuku ni lazima lisafishwe kikamilifu na baada ya usafi huu dawa (disinfectant) itumike ili kuuwa vimelea vya maradhi ya kuku.
-      Weka matandiko kwenye chumba hicho
-      Kama vifaranga ni vingi tayarisha mzunguko kwa kutumia karatasi ngumu isiyozidi urefu wa sentimita 40 endapo kutakuwa na karatasi ngumu, au kona za chuma kwa kutumia kibao chenye pembe tatu ili vifaranga visikaliane kwenye kona hizo.
-      Endapo utatumia taa ya chemli, taa hiyo isafishwe masaa 24 kabla ya kulea au kupokea vifaranga taa moja ya chemli unaweza kutunza vifaranga 50 – 60 kutegemea hali ya hewa ya msimu husika. Endapp jiko la mkaa litatumika katika utunzaji wa vifaranga hakikisha mkaa umeungua na kutoa moto mwekundu ili kuepuka hewa yenye sumu mbaya (carbon monoxide) ambayo inaweza kuua vifaranga. Dalili za sumu mbaya kwenye vifaranga
·         Kupiga kelele  ambayo si ya kawaida
·         Vifaranga kulalia migongo yao
·         Kupata vifo vingi
-      Wakati wa kutunza vifaranga ambao huchukua wiki 3 hadi 4 vifo visizidi asilimia 5 endapo vitatunzwa vizuri
-      Joto litakiwalo katika utunzaji wa vifaranga ni kama ifuatavyo.

Wiki ya                  Nyuzi joto za centigredi
Kwanza                 35
Pili                        33
Tatu                      31
Nne                      29

Lakini kwa kuwa mfugaji hatakuwa na kifaa cha kupimia joto, mwenendo wa vifaranga kwenye banda ni lazima uangaliwe kwa makini kama ifuatavyo:-

Vifaranga kusongamana karibu na chanzo cha joto
Hii inaonyesha kwamba joto halitoshi, ongeza taa

Vifaranga kuwa mbali sana na chanzo cha joto
Hii inaonyesha kwamba joto ni kali sana, punguza taa

Vifaranga kuwa upande Fulani tu wa mzunguko hii inaonyesha upepo unaingia kwenye upande Fulani wa chumba
Funga madirisha au ziba matundu

Kusambaa kwa vifaranga ndani ya mzunguko
Hii inaonyesha joto linatosha na kila kitu kiko sawa

A)   Utunzaji wa asili – njia hutumika kwa vifaranga vichache ambapo temba huachiwa kulea vifaranga vyake. Wakati temba nalea vifaranga vyake utagaji hukoma
B)   Utunzaji kwa kutumia taa- njia hii hutumika endapo mfugaji atakuwa na vifaranga vingi kwa wakati mmoja. Mfugaji ni lazima awe makini sana endapo atatumia njia hii.

Ulishaji wa vifaranga na kuku wanaokua
(i)           Chakula cha kulelea vifaranga (chick mash) – Chakula hiki kina kiwango cha protini kati ya asilimia 18 hadi 20. Walishwe vifaranga kuanzia wiki ya kwanza hadi ya nane. Uzito wa Chakula wa kilo 250 unatosha kulisha vifaranga 100 hadi wiki ya nane.
(ii)          Chakula cha kukuzia (growers mash) – Chakula hiki kina kiwango cha protini kati ya asilimia 13 hadi 15. Walishwe kuku wakuao kuanzia wiki 9 hadi ya 18. Uzito wa Chakula wa kilo 500 unatosha kulisha kuku wakuao hadi kufikia utagaji.
(iii)        Kulisha majani – kuku wapewe majani kama ya mpapai au luseni baada ya umri wa wiki mbili.
(iv)        Maji safi na salama – maji safi na salama ni lazima yawepo kwenye kundi la kuku kila mara. Kwani zaidi ya nusu y uzito wa kuku ni maji. Na maji yasipokuwepo uzito wa kuku utapungua mno.

Kuanzia siku ya 1 hadi wiki ya
a)    4 kilo 1
b)   8 kilo 4
c)    12 kilo 8.5
d)   20 kilo 8 hadi 12
Nafasi ya eneo la sakafu au ardhi kwa kila kuku:
Wiki 1-4 = 15 x 15 cm
Wiki 5-8 = 30 x 30 cm
Wiki 9-12-45 x 45 cm

UMRI KWA WIKI          CHAKULA KWA KUKU/SIKU
1.    Gramu 7 HADI 11
2.    Gramu 7 hadi 11
3.    Gramu 7 hadi 11
4.    Gramu 25 hadi 40
5.    Gramu 25 hadi 40
6.    Gramu 35 – 45
7.    Gramu 35 – 40
8.    Gramu 40 – 60
9.    Gramu 40 – 60
10. Gramu 40 – 60
11. Gramu 40 – 60
12. Gramu 45 – 70
13. Gramu 45 – 70
14. Gramu 45 – 70
15. Gramu 45 – 70
16. Gramu 60 - 90
17. Gramu 60 – 90
18. Gramu 60 – 90
19. Gramu 60 – 90
20. Gramu 110 – 120 haadi kuuzwa


VYAKULA VITUMIKAVYO KATIKA UCHANGANYAJI WA VYAKULA VYA KUKU PAMOJA NA VIPIMO VYAKE KWA KILA AINA YA CHAKULA VYAKULA VITUMIKAVYO:

AINA YA CHAKULA
KIWANGO CHA PROTINI (ASILIMIA)
KIWANGO CHA JUU CHA KUCHANGANYIA
Vyakula vya kutia nguvu mwilini (wanga)


1.    Mahindi
8-9
70%
2.    Shairi
11-16
50%
3.    Ngano
12-13
70%
4.    Mpunga
7-7.3
40%
5.    Mtama
11%
30%
6.    Ulezi
13.3
30%
7.    Mhogo
2.00
30%
8.    Uwele
11-12
30%
Pumba za – Mahindi
-      Ngano
-      Mpunga
10
12-15
11-12
6%
10%
Vyakula vya kujenga mwili – protini
A.   Protini ya asili ya nyama
1.    Dagaa
50-70%
10%
2.    Unga wa nyama
50-53%
10%
3.    Unga wa nyama na mifupa
50-51%
10%
4.    Unga wa damu
80%
5%
5.    Maziwa ya unga
33-34

B.    Protini ya asili ya mimea


1.    Maharage
25%
30%
2.    Soya
46
20%
3.    Mashudu ya alizeti
38-41
20%
4.    ufuta
41
20%
5.    mashudu ya pamba
50
10%
6.    mashudu ya karanga
22.5
20%
7.    mashudu ya nazi
20-21
2%
8.    mashudu ya karanga
45-46
20%
Vyakula vitoavyo madini
Asilimia ya Kalisiamu (calcium)
Asilimia ya Fosforasi (Phosphorous)
1.    unga wa mifupa
23%
12%
2.    Shokaa
30%

3.    Magamba ya konokono


4.    Dicalcium phosphate
24%
18%
5.    Tricalcium phosphate
38%
19%
6.    Magamba yamayai


7.    chumvi


8.    madini kutoka maduka ya dawa


Vyakula vitiavyo vitamin


-      lusina iliyosagwa

2%
-      luseni iliyosagwa

2%
-      unga wa vitamin kutoka madukani





VIPIMO VYA AINA MBALIMBALI VYA VYAKULA
CHAKULA
VIFARANGA
KUKU WAKUWAO%
KUKU WA MAYAI%
1.    Mahindi yaliyosagwa
62.00
46.00
70
2.    Pumba za mahindi
10.00
25.00
-
3.    Mashudu ya pamba
10.00
10.00
10
4.    Unga wa dagaa
6.00
2.50
3.5
5.    Mashudu ya alizeti
7.00
10.50
12.00
6.    Unga wa chokaa
2.00
2.5
1.00
7.    Dicalcium phosphate
1.50
1.50
1.50

8.    Chumvi
0.50
0.50
0.50
9.    Unga wa vitamin
1.00
1.50
1.50
jumla
100
100
100

Mwongozo: Aina ya vyakula vinavyofanana vinaweza kutumika endapo kimojawapo hakipatikani.
Mambo ya kufikiria kwanza kabla ya kuchanganya Chakula cha kuku.
1.    Dhumuni la Chakula kwanza kama kuku wa mayai, vifaranga
2.    Chakula vyenyewe vya kuchanganyia
-      Je vinapatikana kwenye eneo husika
-      Fikiria gharama ya manunuzi ya kila Chakula
-      Baadhi ya vyakula vina chembe chembe za sumu
-      Urahisi wa usagikaji kwenye tumbo la kuku
-      Viini lishe vilivyomo kwenye Chakula husika
3.    Matarajio ya kiwango cha uzalishaji
4.    Mahitaji ya viini lishe mwilini mwa kuku
5.    Urahisi wa vyakula hivyo kuchanyanyika ili kupata mchanganyiko unaofaa kwa kuku husika
La kuzingatia – Chakula chenye uwezo wa kunyonya unyevu nyevu kiwekwe mwisho kabla ya kuchanyanya kama vile chumvi. Pia vitamin na baadhi ya madini yachanyanywe kwanza kwenye pumba au unga uliosagwa au kuparazwa wa nafaka.
Kuku wanahitaji kujengewa banda bora na safi ili wasiathiriwe na madhara mbalimbali kama wanyama wakali, wezi na mabadiliko ya hali ya hewa. Vile vile banda bora husaidia kurahisisha kazi ya utunzaji wa kuku, ni muhimu kujenga banda lenye sifa zifuatazo.
1.    Banda lenye kuingiza hewa safi nay a kutosha
2.    Banda lenye kuingiza mwanga wa kutosha
3.    Banda lenye kuzuia upepo mkali
4.    Banda lisilo ruhusu maji kusimama na kuingia ndani na kwamba imara
5.    Banda liwe rahisi kusafishwa
6.    Banda liwe na eneo la kutosha kulingana na idadi ya kuku
7.    Banda liwe katika eneo linalofikika kwa urahisi
8.    Banda liwe imara na lisiwe la muda mfupi

Vifaa vinavyohitajika katika banda la kuku
Vyombo vya maji vyombo hivi ni kama vya bati, plastiki, madebe, vyungu, sufuria, vibuyu na magogo yaliyotengenezwa vizuri kwa shughuli husika vyombo vya maji kwa ajili ya vifaranga na minimum view na kina kidogo kuepuka vifaranga visizame kwenye maji na kusababisha vifo.

No comments:

Post a Comment