Wednesday, April 1, 2015


NDIGANA KALI (EAST COAST FEVER)
Na Augustino Chengula
Utangulizi
Ndigana Kali ni ugonjwa hatari unaowapata ng’ombe wenye sifa ya homa kali,
kuvimba kwa matezi, upumuaji wa shida na vifo vingi hasa kwa ndama.
Ng’ombe
wa kienyeji hawapati kwa urahisi sana
ugonjwa huu ukilinganisha na wale wa kisasa
na hata madhara yake ni makubwa kwa ng’ombe wa kisasa. Ni ugonjwa
unaoenezwa na kupe wanaojulikana kitaalamu kwa jina la ‘
Rhipicephalus
appendiculatus’
wanao beba vijidudu vya ugonjwa vinavyoitwa
Theileria parva
kundi
la protozoa. Kupe hawa ni wale wanaopatikana kwenye masikio la ng’ombe wakiwa
na rangi ya kahawia (kupe sikio kahawia). Ugonjwa huu unapatikana zaidi katika
maeneo yenye mvua nyingi na joto yanayowezesha kupe hawa kuishi.
Kupe aina ya
Rhipicephal
us appendiculatus
(rangi ya kahawia) wanaobeba wadudu
wa Ndigana Kali. Kushoto ni kupe wa kiume na kulia ni wa kike.
Hawa ni kupe wanao beba wadudu wa Ndigana kali wakilishambulia sikio kwa
kupata chakula, wakati huo huo wadudu wa ugonjwa huacha na
kuenda kwenye tezi
ya karibu ya sikio (parotid) na kisha wadudu kusambaa mwili mzima.
Huu ni ugonjwa muhimu sana Afrika unaosababisha hasara kubwa sana kwa mfugaji
inayotokana na vifo vya ngombe pamoja na gharama kubwa zinazotumika
kukabiliana nao kama
vile dawa ya kuogeshea na miundo mbinu yake, uchanjaji na
gharama za matibabu. Ndigana Kali ni ugonjwa wa Afrika unaoyakumba maeneo
mengi; Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Swaziland, Zimbabwe,
Zambia, Tanzania, Kenya, na Uganda, Burundi, R
wanda, Malawi, Mozambique na
Sudni Kusini. Ugonjwa huu uliweza kulipotiwa kwa mara ya kwanza nje ya Afrika
katika visiwa vy Comoro mwaka 2003 na 2004 ukidhaniwa kupelekwa na ng’ombe
kutoka Tanzania waliopelekwa kibiashara.
Dalili za Ndigana Kali
-
Tangu ku
pe mwenye wadudu aume ng’ombe hadi kujitokeza kwa ugonjwa
huchukua wastani wa siku 8 hadi 12; waweza kwenda hadi wiki 3.

No comments:

Post a Comment