Wednesday, April 1, 2015


KIFUA KIKUU CHA NG’OMBE (BOVINE TUBERCLOSIS)
-
TB
Na Augustino Chengula
UTANGULIZI
Ugonjwa wa
kifua kikuu cha ng’ombe ni ugonjwa hatari sana wenye madhara
makubwa kiafya kwa ng’ombe, mwanadamu na hata katika biashara ya kimataifa. Ni
ugonjwa unaosababishwa vimelea vya bakteria wanaojulikana kwa jina la kitaalam
kama
Mycobacterium bovis.
Kimsingi
ni ugonjwa wa mfumo wa upuuaji unaochukua
muda mrefu (kuanzia wiki chache hadi maisha yote) kujijenga ndani ya mwili tangu
maambukizi hadi kuanza kujitokeza dalili za ugonjwa na kuanza kuambukiza
wanyama wengine (hii ndiyo hatari yake). TB yaweza kuwapata
wanyama wengi
lakini mara nyingi ni ng’ombe na nyati. Mwanadamu hupata ugonjwa wa kifua kikuu
kutoka kwa ng’ombe au mazao yake, lakini pia mwanadamu anauwezo wa
kumuambukiza ng’ombe (Tazama kielelezo hapa chini). Maambukizi yameonekana
pia kwa kondoo, mbuz
i, farasi, nguruwe, paa, mbwa na paka.
TB au Tuberclosis ni neno lilotokana na kutengenezwa kwa viuvimbe kwenye matezi
mwilini ya mnyama mwenye ugonjwa vinavyoitwa ‘tubercles’.
Wadudu wa
kifua
kikuu cha ng’ombe wanafanana na wadudu wa kifua kikuu cha mwanadamu
(
Mycobacterium tuberculosis
), kuku (
Mycobacterium avian
), na ule uliogunduliwa na
Johne (
Mycobacterium avian
subspecies
paratuberculosis
).
Maambukizi
Kasi ya maambuki kutoka myama
mmoja kwenda mwingine ni ndogo na kwa
wastani ni sawa na kusema ng’ombe mmoja mwenye ugonjwa humuambukiza
ng’ombe mmoja mwingine. Hii inafanya milipuko inayotokana na ugonjwa huu
kujitokeza taratibu kadri muda unavyoendelea. Hata bakteria wanaotolewa
nang’
ombe mwenye ugonjwa kupitia matone ya mfumo wa upumuaji huwa kidogo
sana ikilinganishwa na magonjwa mengine kama wa midomo na miguu. Hii inafanya
pia kazi ya utambuzi kuwa ngumu sana.
Ng’ombe hupata maambukizi ya bakteria kutoka kwa ng’ombe mwenye ugonjwa
kwa
kupitia makamasi yenye wadudu au matone yanayodondoshwa na ng’ombe mwenye
ugonjwa akiwa anakohoa. Ng’ombe wanaokaa na ng’ombe mwenye ugonjwa
huupata ugonjwa kwa njia ya kugusana. Ng’ombe mwenye ugojwa akiwa
ananyonyesha anaweza kumambukia mwanawe kupit
ia maziwa. Lakini pia ng’ombe
anaweza kupata maambuki akila malisho yenye bakteria.
Njia kuu ya maambukizi kwa binadamu ni kupitia kunywa maziwa yasiyochemshwa
kabisa au yasiyochemshwa vizuri, kula mazao ya maziwa yaliyotengenezwa na
maziwa yasiyo chemshwa
na kula nyama mbichi au isiyopikwa vizuri. Njia nyingine
ambazo ni ndogo ni pamoja na kupata maambukizi kwa njia ya hewa (kupumua), au
kwa kupitia vidonda (maziwa yenye bakteria yakimwagika kwenye kidonda). Watu
wenye ugonjwa huu wanaweza kusambaza ugonjw
a kwa watu wasio na
ugonjwa
wa TB.
Watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu ni wafugaji na hasa wachungaji wa
mifugo, wanaofanya kazi kwenye machinjio na bucha, madaktari na maafisa ugani
wa mifugo, watafiti wanaofanya kazi na ng’ombe pamoja na waka
guzi wote wa
nyama. Watoto pia wanaweza kupata ugonjwa huu kwa kunywa maziwa
yasiyochemshwa.

No comments:

Post a Comment