Wednesday, April 1, 2015


UGONJWA WA KIWELE (MASTITIS)
Na Augustino Chengula
Ugonjwa wa Kiwele ni ugonjwa ambao si rahisi kuukosa hasa kwa wafugaji wa
ng'ombe wa maziwa, lakini pia ng'ombe wa kienyeji. Ugonjwa huu husabisha
uvimbe, muwasho na
joto kwenye kiwele cha mnyama na usababishwa na aina
nyingi ya wadudu aina ya bakteria.
Madhara ya ugonjwa
:
-
Maziwa kuwa na majimaji au yenye usaha na damu hivyo kufanya yasifae kwa
matumizi ya binadamu na ndama
-
Hata wakati wa matibabu maziwa hayafai
kwa matumizi ya binadamu
-
Gharama za dawa na matibabu zinazopunguza faida ya mfugaji
-
Kupungua kwa utoaji wa maziwa kwa asilimia 70 bila hata mfugaji kujua.
-
Muonekano/mvuto wa ng'ombe huharibika
-
Ugonjwa ukizidi sana ng'ombe huwa hafai tena hasa kama kiwe
le na chuchu yake
vimeharibiwa vibaya na kufanywa auzwe kwa ajili ya nyama
-
Ng'ombe pia anaweza kufa kwa ugonjwa huu
Njia zinazochangia ng'ombe kupata mastitis:
1. Ng'ombe mwenyewe:
-
Vinasaba alivyonavyo ng'ombe vinavyomtofautisha na mwingine vinamchango
m
kubwa wa kumfanya asipate ugonjwa wa kiwele au aupate kirahisi ukilinganisha na
mwingine.
-
Utoaji wake wa maziwa, ng'ombe anayetoa maziwa mengi hupata ugonjwa huu
kirahisi pia
-
Mazingira ndani ya kiwele ni ya joto na virutubisho vingi na hivyo kutengeneza
mazingira mazuri ya bakteria kuzalina kwa wingi na haraka.
-
Maumbile ya kiwele na chuchu huchangia uambukizwaji rahisi wa bakteria
kulingana na yalivyokaa hasa yale yanayoning'inia chini na marefu kiasi cha kujigusa
kwenye miguu ya ng'ombe mwenyewe.
-
Ng'om
be kuwa na magonjwa mengine huchangia kupata ugonjwa wa kiwele
-
Kupungua kwa kinga inayotokana na kuzaa au kufanyiwa upasuaji
-
Lishe duni
2.Njia za ukamuaji
:
-
Ukamuaji waweza kufanyika kwa njia ya mikono au mashine.
-
Ukamuaji unaofanywa na mikono hutegeme
a sana na umakini wa mkamuaji
mwenyewe. Kama mkamuaji atakamua maziwa yote kwa ng'ombe hupunguza
maambuki ya ugonjwa kiwele, la sivyo atasababisha ugonjwa.
Usafi wa mkamuaji ni
muhimu ili kuhakikisha haambukizi ugonjwa kutoka kwa ng'ombe mmoja kwenda
mwing
ine.
-
Ukamuaji wa kutumia mashine ni mzuri lakini kama hewa haijawekwe kisahihi
husababisha uharibifu kwenye chuchu na hivyo kuwa rahisi kwa bakteria wa
ugonjwa wa kiwele kupenyeza.
3. Mazingira ya ukamuaji
:
-
Eneo analokamuliwa mnyama linapaswa kuwa safi,
chuchu za mnyama zinapaswa
kusafishwa kabla ya ukamuaji kuanza ili kuzuia bakteria wasiingie ndani ya kiwele.
-
Eneo analolala mnyama linapaswa kuwa safi ili kuepushe viwele na chuchu
kuchafuka na mbolea inayobeba wadudu wengi wa magonjwa.
-
Mkamuaji anapasw
a kuwa msafi na hata vyombo anavyokamulia viwe safi ili
kuondoa mazingira ya kuzalisha bakteria wa ugonjwa huu
Bakteria wa ugonjwa wa kiwele wanaweza kutoka wapi?
Bakteria wa ugonjwa huu wanaweza kutoka
-
Kwenye kiwele cha ng'ombe aliye na ugojwa
-
Kwenye ma
zingira kama ng'ombe wanapolala, kwenye mbolea, kwenye udongo na
maji yenye wadudu hawa.
-
Kuletwa na wanyama wapya walionunuliwa na kuingizwa kundini
DALILI ZA UGONJWA WA KIWELE
Dalili za ugonjwa wa kiwele zimegawanyika katika makundi makubwa
mawili;
zin
azoonekana kwa macho na zisizoonekana kwa macho.
1.Dalili zinazoonekana kwa macho
-
Kiwele huvimba, huwa na rangi nyekundu, cha moto na huwasha kusababisha
ng'ombe ajikune, na huwa kigumu chote au baadhi ya maeneo
Ng'ombe hukosa hamu ya kula na hunyong'onye
a
-
Maziwa huwa yamevilia (vibonge bonge), hupoteza rangi yake na huweza kuwa na
mchanganyiko wa damu au usaha
Kiwele kilicho vimba na chekundu cha ng'ombe mwenye ugonjwa
2. Dalili zisizoonekana kwa macho
-
Hizi ni dalili zinazoonekana kwa kutumia kifaa maalumu kinachoangalia ongezeko la
seli kwenye maziwa (CMT), kiifaa kinachotumiwa na mfugaji mwenyewe. Vipo vifaa
vingine kama SCC vinavyoangalia ongezeko la seli kama dalili ya ugonjwa huu.
Maziwa ya kila
chuchu huwekwa sehemu yake na tambua yametoka chuchu ipi
MATIBABU YA UGONJWA WA KIWELE
Ugonjwa wa kiwele unatibika na hasa matibabu yakifanywa mapema kabla ya
ugonjwa kuwa sugu. Zipo aina mbalimbali za dawa zinazotumika kutibu ugonjwa
huu. Zipo dawa zi
nazowekwa kupitia mrija wa chuchu na zipo zinazochomwa
kwenye mirija ya damu au kwenye myama. Wasiliana na Daktari wa eneo lako ili
akuelekeze dawa inayofaa kwa mifugo yako.
-
Usisahau kuwa maziwa yenye dawa hayafai kwa binadamu, unaweza kupata
hasara kubwa
sana kwani itasabisha maziwa yote kumwaga au hata kuwazuru
watumiaji kiafya.

No comments:

Post a Comment