Wednesday, April 1, 2015

UFUGAJI WA KWARE SOMO LA UFUGAJI: UZURI WA MAYAI YA KWARE KAMA CHAKULA Katika siku za hivi karibuni ndege aitwae kware ameanza kuwa ndege maarufu katika baadhi ya wafugaji katika nchi yetu na kwa wale ambao walikuwa wakiwawinda porini enzi hizo bado wana imani kuwa ndege huyu hawezi kufungwa kama hatakimbia basi atajiua, lakini kwa wale wanaotaka kumfuga ndege huyu mdogo mwenye mayai matamu ya madoa doa wanaweza sasa inaweza kugeuka chanzo cha mapato na sehemu ya chakula bora kwa familia. Leo ningependa niingie ndani kuwa nini hasa tofauti ya mayai ya kware na yale ya kuku ingawa taarifa nyingi nilizopata kwenye mitandao na kwinginekoinaonyesha tu kwa habari za watu waliopata kutumia mayai kware na kuona umuhimu wake katika afya na baadhi ya tovuti kuongelea tu kwamba mayai haya ni mazuri yanasaidia kwa afya bado kama watu wanaotaka kueleew inakuwa haikidhi haja kuamani tu yakuwa yana saidia katika afya, nikiwa mmojawapo wa watu ambao niliona yanasaidia watu walikuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakiendelea vizuri. Na mpaka sasa mimi napenda kukiita hiki chakula bora na sio dawa kama watu wengi waliotumia wakapata nafuu kwa yale waliokuwa yakiwasibu na wale waliokuwa na dhaifu nyingine katika mwili wakarejea afya maridhawa lakini msimano wangu binafsi napenda kutambua mchango wa haya mayai kama chakula bora. Ndio maana hata Mungu aliamua kuwapa wana waisrael kama chakula kwenye Kutoka 16:13 na mtumishi Daudi anakomelezea kwenye Zaburi 105:40. Sasa kwa kuwa siku zote najua kuwa Mungu hapingani na sayansi kitu wanasayansi wanachofanya nikungudua tu mambo ambayo Mungu ameyaweka kwahiyo ikabidi nitafute kisayansi sasa sisi tunaopenda kuoona na kufanya akili zetu zielewe maana ukielewa jambo kwenye akili yako ni rahisi kufanyia kazi. Katika kutafuta nikasema pamoja na vyanzo vya wataalamu binafsi ningependa kupata vyanzo vilivyo vya kiserekali ambavyo wao hawana upande waliolalia maana hawa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na ajenda zao, Na ndipo nilipopata utafiti wa USDA (United State Department of Agriculture) unaonyesha tofauti za mayai haya kwa kina katika category 78 za nutrients zilizogawanya mayai ya kware yana vitu 31 zaidi ambayo ya kuku hayana kabisa wakati yale ya kuku ya kitu kimoja tu ambacho hakiko kwenye ya kware ambacho naomba nikitaje nacho ni Vitamin K (phylloquinone) na katika hizo 45 vilivyobaki vya kware 42 viko juu na vingine hata mara mbili ya zile za kuku, wakati vya kuku ni 3 vitatu ambayo vimezidi vile vya kware. Angalia link hizo hapo chini kwa number kamili Faida hizi zote tunaweza kupata kama watu wetu watajiingiza katika ufugaji wa ndege huyu ambaye anapatikana sehemu nyingi unaweza kuanza kidogo kidogo mpaka wakafikia mwengi,na kama unavyooana hapo juu unaweza kutengeneza banda rahisi la mbao laini na wafu na kuanzia hapo, ila wawapo wadogo waweke kwenye box na kuwawekea taa kama ufanyavyo kuku.Ufugaji nyuma ya nyumba Naomba niwakilishe nakaribisha maswali comment hapo chini ili tuendelee kujifunza zaidi faida ya ndege huyu na manufaa yake katika maisha yetu Ahsanteni. Michuzi Read more Habari Zinazoendana 2 months ago Mwananchi 24 Jan Wafugaji samaki sasa wapewa somo la ufugaji bora nchini Wafugaji wa samaki nchini wametakiwa kuacha ufugaji wa mazoea ambao huwasababishia hasara, na badala yake washirikiane na wataalumu kubaini mbegu bora na zinazofaa. 3 months ago Vijimambo HABARI NDIYO HII NO SHULE NO CHAKULA KAMA UKUBARI KUUZA GENGE LANGU ONYO: Bila chenyi kamali uwezi kuuziwa kitu chochote hapa 5 months ago Dewji Blog 08 Nov Mayai mabovu yasambaa Dar ! Egg-In-Tray Na Mwandishi wetu AFYA za wakazi wa jiji la Dar es Salaam ziko hatarini kutokana na kula mayai ya kuku yaliyooza, ambayo yameingizwa kinyemela nchini na baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wawekezaji. Mtoa taarifa hii anasema mayai hayo yamekuwa yakisambazwa kwa wingi mitaani huku hatua stahiki hazichukuliwi . Alisema kama Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi itashindwa kuwadhibiti wakezaji hao wasio waminifu wakaingiza mayai hayo kinyume na sharia basi serikali ijiandae kwa fedha nyingi... 6 months ago GPL NI KWELI MAYAI HUSABABISHA UGONJWA WA MOYO? UTAFITI uliofanywa nchini Marekani hivi karibuni unaonesha kuwa katika miaka ya 1950, wastani wa ulaji wa mayai ya kuku ulikuwa mayai 375 kwa mtu mmoja, lakini hadi kufikia mwaka 2007, kiwango hicho kimepungua hadi kufikia mayai 250 tu kwa mtu mmoja, ikiwa ni punguzo la asilimia 33. Sababu moja wapo ya kushuka kwa ulaji wa mayai imeelezwa kuwa, pamoja na sababu zingine, ni imani potofu kwamba mayai husababisha ugonjwa wa moyo na... 6 months ago BBCSwahili 15 Oct Facebook kuwahifadhia wanawake mayai ya uzazi Wafanyakazi wa kike wa Facebook na Apple wanapewa nafasi ya kugandisha mayai yao ya uzazi kwa njia ya maabara ili wafanye kazi mwazo 5 months ago Tanzania Daima 09 Nov Wakazi Dar walishwa mayai mabovu AFYA za wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ziko hatarini kutokana na kudaiwa kula mayai ya kuku mabovu ambayo yameingizwa nchini kinyemela na baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni... 1 year ago Mwananchi 20 Dec Uzuri wa juisi ya miwa Inafurahisha kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi jijini Dar es Salaam wanaouza juisi ya miwa. Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa. Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi. 1 year ago Tanzania Daima 09 Jan Sunfish hutaga mayai milioni 300 kwa mkupuo NI nadra kwa samaki aina ya sunfish kuishi katika makundi. Mara nyingi samaki hawa huishi wawili wawili kama si mmoja mmoja. Hata hivyo tofauti ni pale ambapo wanapotafuta namna ya... Share Share on facebook Share on twitter Share on email Share on print More Sharing Services Top 10 Tanzania Today Today Breaking News,Tanzania

No comments:

Post a Comment